Habari News Tanzania
Halmashauri Kuu ya
CCM ya Taifa inafanya mikutano yake ya
kawaida mara moja kila baada
ya miezi minne,
lakini inaweza kufanya mkutano usiokuwa
wa kawaida wakati wowote endapo
itatokea haja ya kufanya hivyo au kwa
maagizo ya kikao cha juu.
Mkutano wa
Halmashauri Kuu ya Taifa utakaofanyika
katika kipindi cha miezi sita ya mwisho wa kila
mwaka utakuwa pia na kazi maalum ya kupokea
na kujadili taarifa ya utekelezaji wa
Ilani ya CCM unaofanywa na Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mwaka wa fedha uliopita wa Serikali hizo ambao
ulimalizika tarehe 30 Juni ya mwaka unaohusika.
Katika
mikutano yote ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa,
uamuzi utafikiwa kwa makubaliano ya
jumla, au kwa wingi wa kura za Wajumbe waliohudhuria na kupiga kura. Lakini ukitokea uamuzi unaohitajika kutolewa
kuhusu vyombo vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au
vyombo vya Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar au kuhusu muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, uamuzi huo ni lazima upitishwe
kwa azimio lililoungwa mkono na theluthi mbili ya kura za Wajumbe kutoka
Tanzania Bara na theluthi mbili ya kura za Wajumbe kutoka Tanzania
Zanzibar.
Mwenyekiti wa CCM
atakuwa Mwenyekiti waMkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM yaTaifa, lakini
Mwenyekiti wa CCM asipoweza kuhudhuria, mmoja wa Makamu wa Mwenyekiti wa CCM
atakuwa Mwenyekiti wa muda wa Mkutano huo.
No comments:
Post a Comment