Habari wana JF wenzangu, Nimeguswa kuleta uzi huu kwenu baada ya kuona
kama inakuwa mazoea na hakuna anayepiga kelele kuhusu udhalilishaji huu.
Kumekuwa na wimbi la wasanii wa bongo fleva kutoa video zinazoonesha
wanawake wakiwa watupu, tena bila aibu wakitegemea ziangaliwe kwenye
public wakati zipo too pornographic. Huku ni kudhalilisha wanawake, na
ukiangalia asilimia kubwa ya wanaosifia ni wanaume, wakisahau kwamba
wana dada zao, mama zao na binti zao, vipi wangekuwa miongoni mwa hao
wanaojianika utupu, wangesifia the same way? Video hizo ni Zigo wa AY,
Asanteni kwa kuja wa FA, na Achia body wa Ommy Dimpoz, ni udhalilishaji
kwa wanawake na wasipodhibitiwa kweli tunaelekea pabaya. Mamlaka na
taasisi husika hawalioni hili? Taasisi za kutetea haki za wanawake nazo
hazilioni hili? Mwisho naomba Mheshimiwa Nape atusaidie kwa hili.
No comments:
Post a Comment