Saturday, January 23, 2016

Waswahili na utumwa wa simu za mkononi

Habari News Tanzania

Jamani hebu kidogo tutafakari hili, hakuna anayebisha au kukataa kwamba ujio wa simu za mikononi hasa hizi smart phones imesaidia kwa kiasi kikubwa usamabazaji wa habari na utumaji wa taarifa/habari kwa muda mfupi na kwa watu wengi sana, tatizo ninaloliona hasa kwa huku kwetu achilia mbali Africa nzima, tuiangalie Tanzania yetu tu kama mfano, matumizi ya simu yamekuwa kero kubwa sana maeneo mengi tu tunayojishughulisha kutafuta mkate wa kila siku, kuna watu hawafanyi kazi za uzalishaji kutwa na usiku mzima wako kweny instagram, fb , twitter na kwingineko ili mradi tu siku ameimalizia huko, ukiajiri kijana ofisini ndiyo kwanza umempa nafasi kutwa nzima kujipiga picha ku update accounts zake, assignment ulizompa utakuta sababu kibao, nyumbani mboga zinaungua kila siku kisa mke au housegirl yuko facebook!!kwenye magari ya abiria ndiyo usiseme imekuwa kama ushindani, kila abiria akwe amekaa au amesimama yuko kwa fb, insta nk, na ukichungulia hata kwa wizi utakuta hakuna cha maana zaidi ya ku like tu alichokiona!!! na mwingine anadiriki kumpigia simu mwenzie kumlaumu kwa nini haja like picha yake ya leo!!!!!

Sasa huwa najiuliza hivi huu utumwa hivi ni kweli wazungu walituletea ili watupumbaze akili zetu kama tulivyokuwa tunaambiwa zamani? maana nyumbani utagombana na mkeo, housegirl kazi hawafanyi ipasavyo kisa simu, ofisini utagombana na wafanyakazi wenzio au wako sababu simu, kwenye daladala unaweza kutukanwa ukigusa simu ya mtu akiwa ana like!!!!tena ukute ana like upumbavu tu.

Imefikia hatua hata kwenye nyumba za ibada wachungaji na mashekh hawasikilizwi tena na walio wengi waumini wanachat na kusoma habari za mitandaoni!!! huwa wanaitkia tu pale walipokariri lakini mahubiri hawasikilizi tena!!!

Huwa najiuliza hata maisha ya mtanzania ni ya kustaajabisha sana, unakuta mtu yuko tayari asile ila weke bundle ya elfu moja au mbili simu iwe hewani!!! na sasa hivi imekuja hii style ya headphones ndiyo balaa tupu yaani watu wamekuwa kama mazuzu hivi, hadi madereva wanaendesha magari wameweka headphones wanasikiliza redio wakati gari anayoendesha ina radio na hata kanuni za udereva haziruhusu hivyo vitu kwani huwezi kusikia lolote linalohusu chombo unachokiendesha lakini imekuwa ni balaa, abiria, kondakta mpaka dereva wote wamevaa headphones na radio ya gari sauti juu!!!! hapo sasa.
Hii kitu inakera sana, sikatai matumizi ya hivi vitu ila sasa imekuwa too much na inaonesha ulofa wetu ulivyo kwani ikija style nyingine woooooooote wanahamia huko, mzungu anafikiria mambo yake!!!!! 

No comments: