Friday, January 22, 2016

Will Smith kususia tuzo za Oscars

Msanii wa Filamu Will Smith amethibitisha kwamba ataungana na mkewe, Jada Pinkett Smith, katika kususia tuzo la Oscars mwezi ujao.
Msanii huyo anayetambuliwa kwa filamu yake ya ''The Men in Black'' amesema itakua "vigumu" kuhudhuria wakati kujna mzozo kuhusu ukosefu wa uwakilishi wa watu wa tambaka mbali mbali katika uteuzi wa tuzo hilo mwaka huu.
" Hatujihisi vizuri kusimama huko na kusema hii ni sawa,"alimueleza mtangazaji wa kipindi cha Good Morning America Robin Roberts.

Msanii wa vichekesho Chris Rock anakabiliwana miito ya kumtaka ajiondoe kwenye kazi aliyopewa kama mwongozaji wa taratibu za tuzo la Oscas mwaka huu, huku mzozo huo ukiendelea.
Katika mahojiano yaliyotangazwa Alhamisi Smith alisema uteuzi wa mwaka huu ulizingatia "wamarekani wenye mamlaka" na kwa hilo , "kwa kiwango kikubwa , Hollywood iliunda sura ya kufikirika ya uzuru".
Alipoangalia orodha nzima iliyojaa wazungu pekee walioteuliwa kuwania ushindi wa Oscars, aliendelea kusema, "haikuonyesha dhahiri uzuri huo ."

No comments: