Saturday, January 23, 2016

Sakata la Escrow:‘Vigogo Escrow’ kuongoza Kamati za Bunge

Habari News Tanzania

PIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai jana alitangaza majina ya wajumbe wa kamati mbalimbali za Bunge mjini hapa.
Baadhi ya wajumbe wamehamishwa katika kamati walizokuwa awali ikiwemo Kamati ya Hesabu za Serikali ambayo Mwenyekiti wake alikuwa Zitto Kabwe, sasa amewekwa katika Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.
Ndugai alisema orodha hiyo pia imejumuisha wabunge ambao hawakuomba kupangwa katika kamati zozote na wale ambao wameomba kamati moja. Alisema Spika , Naibu Spika , Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kiongozi wa Upinzani ni wajumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge.
Aliwataja wajumbe wa Kamati ya Uongozi kuwa ni pamoja na Spika Job Ndugai (Mwenyekiti), Dk Tulia Akson (Makamu Mwenyekiti), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mwanasheria Mkuu George Masaju, Freeman Mbowe ( Mjumbe wa Kamati ya Bajeti pamoja na Kamati ya Kanuni ya Bunge).
Wengine ni Mwenyekiti wa Haki Maadili na Madaraka ya Bunge, Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Ukimwi, Mwenyekiti Kamati ya Bajeti, Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda Biashara na Mazingira, Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria, Mwenyekiti wa Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa na Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.
Wajumbe wengine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi Maliasili na Utalii, Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu.
Wajumbe wengine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama , Mwenyekiti wa Sheria Ndogondogo, Mwenyekiti wa Kamati za Hesabu na Serikali za Mitaa , Mwenyekiti wa Hesabu za Serikali na Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma.

No comments: