Friday, January 29, 2016

LIVE KUTOKA BUNGENI : SERIKALI ITAKAPOFUTA POSHO ZA VIKAO ZA WATUMISHI WA UMMA, WABUNGE

LIVE KUTOKA BUNGENI : SERIKALI ITAKAPOFUTA POSHO ZA VIKAO ZA WATUMISHI WA UMMA, WABUNGE
“…. Kama moja ya njia za njia Serikali kupunguza matumizi yasiyo ya muhimu kwa kuyaaagiza mashirika ya umma kufuta kabisa posho za vikao na kupunguza posho za kujikimu kwa maafisa wake ili kuonana na zile za watumishi wa Serikali wanaolipwa Shs. 120,000/= kwa maafisa waandamizi wa Serikali.
(WABUNGE WANASHANGILIA KWA KUPIGA MAKOFI NA VIGELEGELE ….)
“…. (mtoa maada anaendelea ....) .... Aidha kwa madhumuni hayo hayo Serikali imeamua kufuta kabisa posho za vikao wanazolipwa wabunge kwa sasa ambayo ni Shs. 220,000/= kwa siku na badala yake imeamua kuwaongezea posho ya kujikimu kutoka Shs. 80,000/= kwa siku wanazolipwa kwa sasa hadi Shs. 120,000/= kwa siku kama ili kulingana na posho wanayolipwa watumishi wengine wa umma ambao malipo yao yanatokana na kodi za wananchi
“Ndugu, wabunge fedha zote zitakazookolwa kutokana na hatua hizi zitaelekezwa katika kuboresha huduma za jamii ikiwemo afya na mpango wa kutoa elimu bure kuanzia shule za awali hadi kidato cha nne.”
(... WABUNGE WANAANZA KUZOMEA KWA NGUVU HUKU WAKIPIGA MEZA NA KUPINGA POSHO ZAO KUFUTWA. WANASIMAMA WAKITAKA MWONGOZO … SPIKA ANAKATAA ….. VURUGU ZINATOKEA NA WENGINE WANAANZA KUTOKA NJE YA UKUMBI WA BUNGE ....)


…… alaaaah! Kumbe ninaota …….

No comments: