Maeneo makubwa ya
mashariki mwa marekani yamefukiwa na theluji kufuatia kuanguka kwa
kiwango kikubwa zaidi cha theluji kuwai kushuhudiwa.
Zaidi ya watu
milioni 80 katika majimbo 18 wameathirika. Usafiri wa reli na ndege
umetatizwa na zaidi ya watu 200,000 kubaki bila umeme.Maeneo mengine yalishuhudia theluji yenye hadi urefu wa mita moja. Utawala katika mji wa New York unasema marufuku ya usafiri inahitaji kuondolewa licha na mji huo kushuhudia theluji kubwa leo jumapili
No comments:
Post a Comment