Habari News Tanzania
Idara ya usalama wa Taifa (TISS) imeundwa kwa sheria ya bunge namba 15 ya mwaka 1996 (Tanzania Intelligence and Security Service act No. 15 of 1996)
iliyosainiwa na Rais Benjamin Mkapa tarehe 20 mwezi Januari mwaka 1997.
Sheria hiyo ndio inayoipa mamlaka Idara ya Usalama wa Taifa kufanya
kazi zake ndani na nje ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, na pia ina
ainisha majukumu, mamlaka na mipaka ya idara ya usalama wa Taifa.
Kutokana na kuwepo kwa sheria hiyo siyo rahisi kwa idara hiyo kufanya
mauaji ya raia wasio kuwa na hatia kwani idara itakuwa inavunja sheria
na kukiuka mamlaka iliyopewa na bunge.
Ni jukumu la idara hii kumchunguza mtu yeyote, kikundi cha watu au taasisi yoyote endapo idara hiyo inayo sababu ya kuamini (reasonable cause) kwamba mtu huyo anahatalisha au ni chanzo cha hatari kwa usalama wa Taifa. Kwa sababu hiyo idara hii inaruhusiwa kuingia (kumchunguza) kwa mtu yeyote, idara yoyote ya serikali, mamlaka yoyote, polisi au 'policing organisation' yoyote.
Aidha idara hii
inao wajibu wa kuzuia vitendo vyote vya kigaidi
(terrorism) vinavyopangwa kufanyika katika ardhi ya Tanzania
bara, Zanzibar na sehemu nyinginezo ambazo ni mali ya jamhuri ya
muungano wa Tanzania ( k.m barozi zetu). Idara inawajibika kufanya
uchunguzi, kuwatambua magaidi, na kuvifahamisha vyombo vingine vya dola
ili kupanga mikakati ya kuwakamata na kuwafikisha mahakamani.
Kutokana
na majukumu ya idara hii, maafisa wa usalama wa Taifa wanalindwa na
sheria na kwamba hawawezi kushitakiwa mahakamani kwa jambo lolote
walilolifanya wakati wa kutekeleza majukumu ya idara ya usalama wa
Taifa.
Idara ya Usalama wa Taifa (Tanzania Intelligence and Security Service) ndiyo idara maarufu na inayoogopwa
sana na wananchi walio wengi. Kutokana na kutoifahamu vizuri idara hii,
wananchi wengi wanaichukia na kuiogopa kwa kudhani kuwa hii ndiyo idara
inayotumika katika kuwaua na kuwatesa watu wenye mlengo na mawazo
tofauti ya kisiasa hususan viongozi wa vyama vya upinzani. Kwa mfano,
katika hali isiyo ya kawaida idara hii ilitajwa sana na kuhusishwa na
vifo vya aliyekuwa katibu mkuu wa CCM, marehemu Horace Kolimba,
aliyekuwa waziri wa mipango na uchumi wakati wa serikali ya wamu ya pili
Profesa Kigoma Ali Malima, na hata mzee Mahimbo aliye fariki hivi
karibuni kwa ajali ya gari. Hata hivyo hakuna ushahidi wowote unao
onesha au kuthibitisha kwamba idara hii ilihusika kwa namna moja au
nyingine na vifo hivyo.
Naibu Mkurugenzi Jacky Nzoka |
Hata
hivyo, kama ilivyo kwa jeshi la wananchi wa Tanzania na Jeshi la
Polisi, kadhalika idara hii INARUHUSIWA kutumia nguvu ya ziada
(Reasonable force) katika kuwazuia maadui kumdhuru Rais wa Jamhuri ya
muungano wa Tanzania, viongozi wengine na wananchi wote wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania. Kwa msingi huo, maafisa wa Usalama wa Taifa
wanaweza kutumia nguvu au silaha yoyote inayofaa (reasonable force)
katika kuwazuia magaidi, majasusi au maadui wanaotaka kufanya hujuma.
Hata
hivyo nguvu hiyo ni lazima iwe inayofaa na isiyozidi kupita
kiasi (reasonable force). Endapo adui atakuwa na silaha, basi maafisa wa
Usalama wa Taifa watatumia silaha kumkabili adui hiyo. Ndio maana mtu
aliyempiga kibao Rais mstaafu Ali Hassan Mwnyi hakuuawa kwa kupigwa
risasi, bali alikamatwa na kushitakiwa.
Pamoja
na idara hii kusajiliwa kisheria mwaka 1996, idara hii ilkuwepo tangu
wakati wa utawala wa Mwalimu Julius Nyerere ambapo ilikuwa ikifanya kazi
chini ya mwamvuli wa ofisi ya Rais. Pengine kitu kilicho pelekea
kusajiliwa kwa idara hii ki sheria ni mabadiliko ya mfumo wa kisiasa na
uchumi yaliyotokea duniani mwishoni mwa miaka ya 1980 na kuingia
Tanzania kwa kasi miaka ya 1990. Mabadiliko hayo na hasa kuanzishwa kwa
mfumo wa vyama vingi viliiweka idara hii katika hali ngumu ki utendaji
kutokana na viongozi wengi wa vyama vya siasa kuamini kuwa idara hiyo
ina kilinda chama tawala.
Baadhi
ya wakurugenzi waliopata kuongoza idara hii ni marehemu Emilio Mzena
(mkurugenzi wa kwanza) ambae alijipatia umaarufu mkubwa miongoni mwa
wananchi kiasi cha kujulikana kwa jina la 'Mr Serikali'. Wengine ni
marehemu Dr Laurence Gama, Mzee Hans Kitine, marehemu Luteni Jenerali
Imran Kombe, na Colonel Abson. Wakati wa uongozi wake Colonel Abson
aliiboresha idara ya usalama wa Taifa na kuhakikisha muswaada wa kuundwa
kwa idara ya usalama wa Taifa kisheria unapelekwa bungeni na hatimae
kusainiwa na Rais Mkapa. Hivi sasa Idara ya Usalama wa Taifa inaongozwa
na Rashid Othman (Mkurugenzi mkuu) akisaidiwa na wakurugenzi wengine
wanao ongoza kurugenzi ndogo.
Majukumu ya idara ya usalama wa Taifa.
Ni jukumu la idara hii kumchunguza mtu yeyote, kikundi cha watu au taasisi yoyote endapo idara hiyo inayo sababu ya kuamini (reasonable cause) kwamba mtu huyo anahatalisha au ni chanzo cha hatari kwa usalama wa Taifa. Kwa sababu hiyo idara hii inaruhusiwa kuingia (kumchunguza) kwa mtu yeyote, idara yoyote ya serikali, mamlaka yoyote, polisi au 'policing organisation' yoyote.
Kukusanya
taarifa za ki intelejensia na ki usalama, kuzichambua na kuzitumia
taarifa hizo kuzuia vitendo vyovyote vya ki adui vinavyoelekezwa kwa
jamhuri ya muungano wa Tanzania. Kumshauri Rais na Mawaziri kuhusu
maswala mbali mbali ya ki usalama. na kuvifahamisha vyombo vingine vya
dola kuhusu uwezekano au kuwepo kwa vitendo vya ki adui katika jamhuri
ya muungano wa Tanzania. Idara hii ndio iliyopewa jukumu la kuilinda
jamhuri ya muungano wa Tanzania kutokana na vitendo vyote vya ki adui
ikiwa ni pamoja na ujasusi (espionage), uhujumu (sabotage) ugaidi
(terrorism) na uhaini na uzandiki (subversion)
Kwa
sababu hiyo, idara ya usalama wa Taifa inao wajibu wa kuilinda na
kuitetea serikali ILIYO CHAGULIWA na wananchi wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania ili isiondolewe madarakani KINYUME cha sheria. Idara inatakiwa
kuwadhibiti watu au kikundi cha watu wanaopanga mapinduzi, wanaotoa
vitisho au maneno ya kuwashawishi wananchi kuipindua serikali
(uzandiki) au namna nyingine yoyote ya kuiondoa serikali pasipo kupiga
kura kama inavyo agizwa na katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
DCI Robert Manumba |
Idara
hii pia inalo jukumu la kuchunguza, kugundua na kuzuia njama zozote
zinazopangwa na mtu binafsi, kikundi cha watu, au nchi jirani zenye
lengo la kuleta machafuko, mauaji au maangamizi ya aina yoyote kwa
wananchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa lengo la kujipatia
mafanikio ya kisiasa, ki uchumi, au kijamii ndani au nje ya jamhuri ya
muungano wa Tanzania. Idara ya usalama inatakiwa kuwatambua watu
wanaopanga mipango hiyo na watu au serikali zinazo wasaidia katika
kutekeleza mipango hiyo, Kuchunguza vitendo vinavyofanywa na serikali za
nje, asasi zisizo za kiserikali na wageni ili kubaini njama zinazounga
mkono au kusaidia vitendo vya kijasusi au hujuma katika nchi yetu.
Aidha
ni wajibu wa idara ya usalama wa Taifa kuhakikisha kuwa wananchi wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania wanaendelea kuishia kwa utulivu, amani
na mshikamano kwa kuchunguza na kubaini matatizo mbali mbali yanayo
wakabili wananchi na kuishauri serikali iliyopo madarakani namna ya
kuondoka kero zinazo wakabili wananchi.
Idara
hii pia ndio yenye jukumu la kuwalinda viongozi wote wa kitaifa ikiwa
ni pamoja na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais,
Rais wa serikali ya baraza la mapinduzi Zanzibar, na wengineo ambao
idara kwa sababu moja au nyingine itaona wanafaa kupewa ulinzi.
Aidha idara ya usalama wa Taifa inawajibika kukusanya taarifa zote za kiusalama ndani na nje ya nchi na kuishauri serikali (Rais) kufanya maamuzi mazuri na yenye faida kwa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Aidha idara ya usalama wa Taifa inawajibika kukusanya taarifa zote za kiusalama ndani na nje ya nchi na kuishauri serikali (Rais) kufanya maamuzi mazuri na yenye faida kwa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
29 comments:
Je nafasi za kazi katika idara hii ya usalama wa Taifa zinatangazwa wapi? na ni kwa watu gani?
ninayo hamu au shauku kubwa mno ya kuitumikia nchi yangu ktk idara hii.bali sijuh vigezo,au jinsi ya kujiunga,
Idara hii ninandoto nayo sana kuifanyia kazi lakini sijajua taarifa za kujiunga
nina hamu sana ya kufanya kaz katika idara hii naweza vipi kuungana na nyie
ok,pongezi kwa idara ya usalama
usiweke picha
nina hamu,amasa, moyo, na upendo na wizara ya usalama wa Taifa kwasababu ninaipenda nchi yangu Tanzania kwahiyonina shauku ya kufanya kazi katika wizara hii
na sasa nimeanza kujiungz na jeshila kujenga Taifa ila ndoto zangu ni kufanya kazi katika wizara ya mambo ya ndani hususani usalama wa Taifa
HONGERA TISS
Bado idara hii ya usalama wa taifa inaupungufu wa informants katika ngazi za chini za kiutawala! binafsi nimejaliwa kuwa na hisia kali za kuweza kulitambua jambo kabla halijatokea na kama kuna jambo lishatokea huwa ni mwepesi na mtulivu ktk kutafuta kiini cha tatizo na kushauri nini kifanyike! mimi mzalendo raia wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Je, matukio mnayohusishwa nayo kama lile la kutekwa na kuteswa kwa m/kiti wa madaktari, Ulimboka pia m/kiti wa jukwaa la wahariri ndugu Kibanda, ni kweli mmehusika nayo kwani kazi zao zinaigusa Serilali moja kwa moja? Napenda kufahamu kihusu hayo
Ilikuwaje idara hii haikuwajibika katika suala la watu kutuibia mamilioni ya fedha kutoka benki kuu? Je, wizi huu haukuwa hujuma ya wazi dhidi ya Tanzania? Nakumbuka Nyerere alikuwa macho sana na wahujumu uchumi, hata kama hapa na pale alizidisha mambo. Lakini leo je, idara hii imechukua hatua zipi dhidi ya hao walioiba benki kuu? Ningependa kupata maelezo, maana kwangu ni kitendawili.
Mnatekeleza wajibu wenu kwa asilimia kathaa ongezeni jitiada kukabiliana na wavunja sheria
thanks for information
Mimi ni meja wa jeshi(jwtz) kwa imani yangu ninavyojijua nina vigezo vya kuitumikia nchi yangu kupitia idara hii. Nina ndoto hizo toka zamani lakini sehemu ya kuanzia sina.ninaomba nielekezwe kujiunga kama itakubalika.nahofia kuweka contacts zangu hapa emails kwa kuwa naamini kwa sasa si vema. Nipeni nafasi nitumikie nchi yangu kwa huo nao pia kama ninavyotumikia upande niliopo sasa.
kwani si mnajuana mkuu, ungewauliza wao... kufikia ngazi ya umeja wa jeshi nina imani una abc za hao jamaa.
Naitwa getrude,hongereni kwa kazi nzuri,nimekuwa nikitamani kuwa mmoja wenu toka nikiwa darasa la saba hadi sasa nimemaliza chuo na nipo na mambo yangu sijafanikiwa.kama kuna uwezekano wa kuwa mmoja wenu basi,naomba info kutoka kwenu kwenye email address yangu asseygetrude@yahoo.com.
hongereni kwa kazi mnayo ifanya(kulinda usalama wa nchi) napenda nami niwe miongoni mwa wafanyakazi wa usalama
Hongereni sana kwa kazi kubwa mnayoifanya kwa kulilinda Taifa letu zuri la Tanzania, HONGERENI, na mimi pia nimekuwa na ndoto hii ya kufanya kazi katika idara hii muhimu kwa Taifa letu, mimi kwa taaluma ni mtaalamu mifumo ya computer na mawasiliano yake, kama kuna utaratibu wa kujiunga na idara hii ningependa kujiunga nayo, kwa taarifa yoyote naomba nijulishwe kwa email hii:- rsrmtg@yahoo.com Nawapongeza sana kwa kila kazi mnayoifanya kama wajibu wenu kwa Taifa hili.
Kujichomoza kwa mikono ya toka nje ya mashirika ya kijasusi kama FBI,M16 kunahatarisha idara yetu ya usalama kuweka siri zetu kwa nchi kama marekan kwani wanajipambanua na sera yao kama "wana maslahi ya kudumu na si urafiki au uadui" nadhani kama tungekuwa na idara ya usalama ya nje basi ingeweza tahadharisha idara ya usalama ya ndani ya nchi
Napeipenda sana idara hii yenye kazi ngumu hasa nyakati hizi za utandawazi.
Big up TISS
all the best for the country
ILIKE MORE MORE TO BE AMONG OF THE INTELLIGENCE
I DESIRE TO BE YOUR WORK MATE. HOW CAN I GET CONNECTED WITH YOU?
Watanzania wengi sana tunahamu ya kuitu mikua nchi yetu lakini vigezo na jinsi ya kujiunga ni tatizo mfano mimi naomba kupatiwa maelezo
Mbona author hajibu hoja za wachangiaji hasa jinsi wanavyowapata wafanyakazi wapya?
Ninafanya degree ya philosopy naweza kufanya kaz mahali hapa?
Mimi nimebahatika kuona utendaji wa idara hii ktk nyakati zote za viongozi waliopita ..nidhamu sasa hivi hakuna maafisa wanajitangaza kwenye bar..kwamba wao ni kina nani it is pathetic. ..intelligence officer anatakiwa kuwa kama ghost
Post a Comment